Taarifa ya Habari 18 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri mkuu wa China Li Qiang ameondoka Canberra baada ya siku yakihistoria ya mazungumzo yakidiplomasia ndani ya bunge la taifa.


Kumbukumbu kuhusu makubaliano ya biashara huru kati ya China na Australia, mabadiliko ya mazingira, elimu, utafiti, mazungumzo yakimkakati kuhusu uchumi pamoja na ushirikiano wakitamaduni zilitiwa saini katika mikutano hiyo. Waziri Li alikiri kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na misuko suko katika muongo ulio pita ila, amesema ana amini sasa unaelekea katika mwelekeo mzuri. Wakati huo huo, waandamanaji walijumuika nje ya bunge la taifa ambako wanao unga mkono serikali ya China wali rudia kauli ya waziri Li, wakati wanao pinga chama chaki komunisti cha China walisema serikali ya Australia inahitaji fanya mengi zaidi kuiwajibisha.

Wafanyakazi muhimu hivi karibuni wanaweza stahiki kupokea viwango vya ruzuku za kodi jimboni New South Wales. Kiongozi wa NSW Chris Minns ametoa maelezo ya mipango yaku wahudumia wauguzi, wahudumu wamagari ya dharura, walimu, wahudumu wa afya washirika, jeshi la polisi pamoja na wazima moto kwa viwango vya ruzuku. Kitengo cha maendeleo ya makazi ya serikali, Landcom, kita nunua sehemu nne zakujenga zaidi ya nyumba mpya 400 zaku kodi katika miaka mitatu ijayo.

Watu watatu wamefariki katika ajali mbaya ya barabarani iliyo tokea katika eneo la Western Downs Region jimboni Queensland. Mwanaume mmoja na watoto wawili wali uawa baada ya gari lao kugongana na gari lingine, katika mji wa kijijini wa Jimbour East asubuhi ya Jumatatu 17 Juni. Mwanamke, ambaye alikuwa pia ndani ya gari ndogo amepelekwa hospitalini akiwa katika hali mahtuti. Derava wa gari la pili ambaye ni mwanaume, naye pia ame pelekwa hospitalini lakini hana majeraha yoyote yanayo tishia maisha.

Raia wa Malawi walikusanyika kuomboleza kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Saulos Klaus Chilima huku kukiwa na ulinzi mkali siku ya Jumatatu. Siku moja baada ya watu kutoka kwenye kijiji chake kuanzisha maandamano kuhusiana na majibu ya serikali kwa ajali ya ndege iliyomuua makamu huyo wa rais na watu wengine wanane.
Chilima mwenye umri wa mika 51, amezikwa katika kijiji chake cha Nsipe kilichopo katika wilaya ya Ntcheu, kiasi cha kilometa 160 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Lilongwe.

Mishahara ya wabunge nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imepunguzwa ili kuweka usawa wa baina ya malipo miongoni mwa wafanyakazi katika sekta ya umma, katika taifa hilo linalokabiliwa na mgogoro wa kiuchumi. Kwa miaka mingi ndipo wabunge walikuwa wakipokea mshahara uliozidi ule wa watumishi wengine. Kwa hivyo ndoto ya kila mkongo ilibaki tu ni kuwa mubunge kabla ya kufa. Hatua hii ni kufuatia vuguvugu lililoendeshwa na wanasiasa kutoka vyama vya upinzania nchini humo ambao walitaka mishahara ya wabunge kupunguzwa ili kupunguza uzito wa matumizi ya fedha za umma.

Waziri wa Utumishi wa Umma, Moses Kuria, ameunga mkono bajeti mpya iliyosomwa Juni 13, 2024 na Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u akisema itawezesha Kenya kulipa madeni inayodaiwa na kukoma ukopaji. Akisoma Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2024/25 mnamo Alhamisi, Waziri wa Fedha hata hivyo alisema ina pengo la Sh597 bilioni.
Waziri alifafanua kuwa pengo hilo litajazwa kupitia ukopaji kutoka mashirika ya humu nchini (Sh263 bilioni) na mataifa ya kigeni (Sh333 bilioni). Hata hivyo idadi kubwa ya wananchi wa Kenya wamepinga bajeti hiyo, wakiwataka wabunge wao wapiga kura yakuto ipitisha bungeni. Baadhi ya wakenya wana jiandaa kufanya vikao nje ya bunge la taifa ya Kenya kuwashinikiza wabunge wakati wa kujadili nakupigia bajeti hiyo kura.

Share