Taarifa ya Habari 2 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Australia itatuma wajumbe New Zealand kujadili uwezekano wa ushirika wakijeshi katika muungano wa AUKUS.


Mawaziri wa maswala yakigeni na ulinzi wa nchi zote mbili walifanya mazungumzo jana Februari mosi, walijadili ushirikiano wa karibu katika ulinzi. Nchi zote mbili zimesema kuongeza kizuizi kuwa ni muhimu kwa kile pande zote zinakubali, ni moja ya changamoto ya mkakati katika muongo. New Zealand imeonesha nia yakujiunga na kitengo cha pili cha AUKUS, ambayo huzingatia kuchangia teknolojia ya hali ya juu.

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton ame toa vidokezo imara kuwa chama chake cha Liberal hakita zua pingamizi dhidi ya mageuzi ya chama cha Labor kwa awamu ya tatu ya makato ya kodi. Serikali ya Albanese imevunja ahadi ya uchaguzi, kwa kufanya mageuzi kwa sera yakugawanya mpango wa makato ya kodi katika vitengo vyote vya kodi.
Serikali ita hitaji msaada kutoka chama cha mseto au, kutoka kwa wabunge huru kupitisha muswada huo.

Chama cha Greens kimesema takwimu mpya kuhusu uchumi, zinaonesha serikali ya shirikisho haifanya vyakutosha kwa sera ya nyumba haswa kwa wapangaji. Wakati serikali ina pigia debe takwimu nzuri kuliko ilivyo tarajiwa kuhusu mfumuko wa bei, moja ya vitu muhimu vinne vinavyo changia kwa ongezeko hilo, ilikuwa ni bei ya watumiaji kwa gharama za nyumba.

Umoja wa Mataifa na serikali ya Somalia wameanzisha ombi la dola bilioni 1.6 kwa ajili ya kushughulikia changamoto za kibinadamu nchini Somalia. Mpango wa utekelezaji wa mahitaji ya kibinadamu ni kutoa misaada ya kuokoa maisha kwa zaidi ya Wasomali milioni tano mwaka huu.

Wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete Jimboni kivu Kaskazini na jiji la Goma likikabiliwa na kitisho kikubwa kutoka kwa waasi wa M23, utawala wa kijeshi wa mkoa huo umechukua hatua za kiusalama huko Goma. Sasa, kila mtu anayeingia au kutoka jijini lazima awe ameandikishwa, kulingana na uamuzi uliotangazwa jana Jumatano na Gavana wa Kivu Kaskazini, Jenerali Peter Cirimwami. Wageni wapya wanapaswa kuorodheshwa, na orodha hiyo kuwasilishwa kila asubuhi kwa baraza saa nne.

Wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya sheria, imeelezwa bado upo uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria katika maeneo ya ardhi, matuzo ya watoto na ndoa, huku maeneo hayo yakitajwa yana mgogoro mkubwa. Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini Tanzania kilichofanyika jijini Dodoma yaliyopo makao makuu ya chama na serikali. Rais Samia ameitaka wizara ya sheria na katiba kuhakikisha inashirikiana na wadau, katika kuimarisha suala zima la utolewaji wa haki katika maeneo hayo.




Share