Maelfu ya wakaazi wa Victoria wanaendelea kuwa waathiriwa wa uvamizi wa nyumbani unao fanywa na vijana wanao iba magari, wakati jeshi la polisi lina husisha uhalifu huo na haraka zaku tafuta umaarufu katika mitandao yakijamii. Jimbo la Victoria lilirekodi idadi ya visa 5900 vya wizi uliokithiri manyumbani katika mwaka wa 2023, idadi hiyo ikiwa ni zaidi ya mara mbili kutoka muongo uliopita wakati wahalifu ambao ni vijana wakihusika kwa ongezeko la visa hivyo. Katika visa hivyo 5900, takriban idadi ya uhalifu 3800 bado hauja tatuliwa.
Nguvu kazi mpya jimboni Victoria ita chunguza matangazo feki ya nyumba zaku kodi na zile ambazo hazi kidhi viwango fulani. Nguvu kazi hiyo ita imarisha mamlaka ya uvunjaji wa sheria wa wamiliki wa nyumba pamoja na mawakala wa nyumba ambao hawa wasilishi hela za dhamana yakukodi nyumba.
Wagomea wa uchaguzi wa Tasmania wafanya kampeni za mwisho kabla ya uchaguzi wa kesho 23 Machi jimboni humo. Chama tawala cha Liberal kina wania muhula wa nne mfululizo, wakati chama cha Labor kina tumai kuingia uongozini baada ya muongo mzima ndani ya jangwa la upinzani. Tasmania kwa sasa ndilo jimbo pekee au wilaya nchini Australia ambalo lina serikali ya Liberal.
Chama tawala Afrika Kusini kimekwenda mahakamani kujaribu kukizuia chama kipya cha upinzani kushiriki uchaguzi utakaofanyka mwezi Mei. Uchaguzi mkuu wa taifa wa Mei 29 unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kuwahi kutokea, utafiti ukipendekeza kuwa chama cha ANC kitashinda chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu demorasia ianze mwaka 1994. Sasa, chama cha upinzani kinachoitwa uMkhonto weSizwe, au MK kwa kifupi , kimeikasirisha ANC kwa kujipa jina linalotokana na kitengo cha kijeshi cha ANC ambacho kilipigwa marufuku, kiliundwa na Nelson mandela na kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi. Rais wa zamani Jacob Zuma, shujaa wa ANC, amekiunga mkono chama cha upinzani na kuongeza majeraha tu, na ANC kimemsimamisha.
Mawaziri wa serikali kutoka mataifa matano ya Kiarabu wamekutana na maafisa wa Palestina hii leo mjini Cairo kujadiliana mzozo wa Gaza. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema kabla ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwamba mawaziri hao walijadiliana umuhimu wa juhudi za kusimamisha vita vya Gaza na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na kuhakikisha ufikishwaji wa misaada. Msemaji wa wizara hiyo Ahmed Abuzeid ameandika kwenye mtandao wa X kwamba mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Saudi Arabia, Qatar na Jordan pamoja na Waziri wa uhusiano wa kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Mamlaka ya Palestina.
Baadhi ya hospitali za umma zimeshuhudia shughuli zao zikipungua siku ya Alhamisi nchini Kenya, zaidi ya wiki moja baada ya kuanza kwa mgomo wa kitaifa wa madaktari wakitaka mazingira bora ya kazi na nyongeza ya mishahara. Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU), pekee katika sekta ya matibabu yenye wanachama zaidi ya 7,000, ulizindua maandamano haya mnamo Machi 13. "Serikali haijaonyesha nia ya kuondokana katika hali hii," naibu katibu mkuu wa KMPDU Dennis Miskellah ameliambia shirika la habari la AFP.