Taarifa ya Habari 26 Disemba 2024

Bench - Swahili.jpg

Mamlaka wa Urusi na Australia wachunguza ripoti kuwa, raia wa Australia amekamatwa akipigania Ukraine.


Msemaji wa Wizara ya maswala ya kigeni wa Urusi, Maria Zakharova, amesema wanadiplomasia wa Australia wame zungumza na Moscow kuhusu swala hilo. Katika mwanzo wa 2022, Idara ya maswala yakigeni na biashara ya Australia, ilitoa ushauri wa usafiri ukiwahamasisha wa Australia wasi safiri nchini Ukraine pamoja nakumulika hatari zaki sheria zakushiriki katika mgogoro huo. Jeshi la polisi la shirikisho la Australia limeonya pia kuwa wa Australia wanao shiriki katika migogoro ng’ambo, wanaweza funguliwa mashtaka chini ya sheria za Australia.

Mazingira hatari ya moto yanatarajia kukabili majimbo kadhaa wakati, ukanda wa kusini mashariki unajiandaa kwa wimbi la joto siku yakufungua zawadi inayo julikana kwa kimombo pia kama Boxing Day. Upepo wa uharibifu na hatari kubwa ya moto, umetabiriwa kwa leo Disemba 26, joto, hali ya hewa kavu ina athiri Victoria, kusini magharibi New South Wales, na maeneo ya mashariki Kusini Australia.

Uchumbuzi wakitaifa unadokeza kuwa jimbo la Victoria lita jiunga na jimbo la New South Wales kama maeneo muhimu yakuwaniwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Upendeleo wa serikali ya Labor kwa kura ya kuungwa mkono kwa vyama viwili, imepungua nakuwa sawa na asilimia 50 na upinzani wa mseto.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewaachilia huru raia 14 kati ya 17 wa China waliokamatwa kwa tuhuma za kuendesha mgodi wa dhahabu kinyume cha sheria. Walikamatwa wiki iliyopita pamoja na wengine kutoka Kongo na Burundi kwa kushindwa kuonyesha nyaraka muhimu wakati wa operesheni dhidi ya uchimbaji haramu wa madini.

Nchini Kenya, wasiwasi unaongezeka kuhusu msururu wa utekaji nyara na visa vya watu kutoweka unaodaiwa kutekelezwa na polisi katika wiki za hivi karibuni. IPOA, Halmashauri ya utendakazi wa polisi, imepaza sauti katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumatano, Desemba 25. Taasisi hiyo inatangaza kuwa imeanzisha uchunguzi. Kutoweka kwa watu wawili kumewakasirisha Wakenya kwenye mitandao ya kijamii katika siku za hivi majuzi. Peter Muteti na Billy Mwangi, vijana wawili maarufu kwenye mtandao wa kijamii wa X, walitekwa nyara mwisoni mwa juma lililopita, na kuingizwa kwa nguvu ndani ya gari na watu wasiojulikana.

Share