Chama cha The Greens kime omba mageuzi ya ziada yafanyiwe kwa mageuzi ya pendekezo la awamu ya tatu ya makato ya kodi ya serikali ya shirikisho. Chini ya mfumo huo uliobadilishwa, mtu yeyote anaye lipwa nchini ya $150,000, atapokea makato makubwa zaidi ya kodi wakati wanao lipwa hela zaidi watapokea kiwango kidogo cha makato ya kodi kuliko ilivyo kuwa ime ahidiwa kabla.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameyapongeza maendeleo ya ujenzi wa njia ya Lobito, kiungo muhimu cha reli cha kusafirisha nje nje vyuma kutoka katikati ya ukanda wa shaba barani Afrika, wakati wa ziara nchini Angola siku ya Alhamisi.
Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch Alhamisi limelishtumu jeshi la Burkina Faso kuua takriban raia 60 katika mashambulizi ya ndege isiyokuwa na rubani ambayo serikali ilisema ilikuwa inawalenga wanamgambo wa kiislamu.
Mahakama moja ya Ghana Jumatano iliwahukumu kifo watu sita, wakiwemo wanajeshi watatu wanaoshutumiwa kuhusika katika njama ya kupindua serikali ya nchi hiyo miaka mitatu iliyopita.