Serikali ya shiriksiho inatupilia mbali wasiwasi kuhusu ongezeko kwa bei za viza kuwa hali hiyo ita athiri uchumi. Gharama ya viza kufanya kazi wakati wa likizo, itaongezekwa kwa $130 mwaka mpya wa fedha utakapo anza Jumamosi ambayo itakuwa Julai mosi.
Serikali ya ki-Conservative ya Waziri Mkuu Rishi Sunak inataka kuwapeleka maelfu ya wahamiaji zaidi ya kilomita 6,400 kwenda Rwanda kama sehemu ya makubaliano na nchi hiyo ya Afrika ya kati yaliyofikiwa mwaka jana.
Rais wa Kenya William Ruto ametia saini kuwa sheria mswada wa kwanza wa fedha wa serikali yake, unaolenga kuongeza mapato kwa kutoza kodi katika bidhaa kadhaa bila kujali ukosoaji kwamba ongezeko hilo la kodi litasababisha matatizo mengi zaidi ya kiuchumi kwa wananchi.