Kundi linalo wakilisha madaktari nchini Australia linaomba mageuzi kwa mfumo wa Medicare, ambao kundi hilo limesema hauja badilika tangu mfumo huo ulipo anzishwa mnamo 1984, ili kuendana na mabadiliko yamahitaji ya umma.
Kikao cha uchunguzi wa bunge kime elezwa viwango vya vijana wanao fungwa nchini Australia, vimefika katika viwango vya janga na vina hitaji umakini wa haraka.
Serikali ya Rwanda Jumapili imekubaliana na pendekezo la kufanyika kwa mkutano utakaosimamiwa na SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kujadili mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku Tanzania ikitangaza pia kwamba wanajeshi wake wawili waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni.
Maafisa wa Uganda wanajiandaa kupeleka chanjo ya majaribio kama sehemu ya juhudi za kukomesha mlipuko wa Ebola katika mji mkuu, Kampala, afisa mkuu wa afya amesema siku ya Jumapili.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.