Taarifa ya Habari 3 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mamilioni yawa Australia wata pata nyongeza ya asilimia 3.75 kwa mishahara yao, baada ya tume haki ya kazi kutoa uamuzi wake wa tathmini ya mwaka ya malipo.


Nyongeza hiyo ya mishahara itaanza kutumika kuanzia Julai 1, na mtu yeyote anaye pokea kima cha chini cha mshahara ata pokea nyongeza hiyo. Tume ya Haki Kazini, ime amua kuongeza mishahara chini kidogo ya mfumuko wa bei, ambayo ilikuwa asilimia 4.1 katika mwisho wa robo ya Aprili.

Waziri wa maswala ya kigeni Penny Wong amesema serikali inakaribisha usitishwaji wa mapigano pamoja na pendekezo lakuachia huru mateka ambayo ime ungwa mkono na Rais wa Marekani Joe Biden. Akizungumza katika kikao cha makadirio ya Seneti, Penny Wong ame rudia wito wa seriklai kwa serikali ya Israel ikubali wito wakusitisha mapigano ili mateka waachiwe warejeshwe na raia wa Palestina wapate kinga dhidi ya janga la ziada. Pendekezo hilo ambalo Marekani inasema lilitoka kwa serikali ya Netanyahu, inasema inahitaji kazi ya ziada, ni mpango wenye awamu tatu zinazo jumuisha, kupata makubaliano, kuachiwa huru kwa mateka wa Israeli nawa Palestina pamoja na kukomesha uhasama. Bi Wong amesema kuwa tisho la Peter Dutton kuondoa AUstralia katika mahakama ya jinai ni kutojali na kudhoufisha majaribio ya kukuza utaratibu unao zingatia sheria.

Naibu waziri wa ulinzi Matt Thistlethwaite amekataa ripoti zinazo onya kuwa Australia haita weza ongeza ulinzi wake kwa wakati wa vita. Uchambuzi kutoka ripoti ya taasisi ya sera ya mikakati ya Australia, ilipata kuwa licha ya ongezeko ya hela taslim milioni 50 katika muongo ujao, uwekezaji wa ulinzi unahitajika kuhakikisha Australia ina uwezo kama hali kandani ina dorora haraka. Bw Thistlethwaite amesema matokeo ya ripoti hiyo kimsingi siya kweli, akidokeza kwa ongezeko la bajeti ambalo lime elekezwa kuimarisha uwezo wa jeshi katika muongo ujao.

Imefahamika kuwa jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linahitaji angalau dola milioni 56 kuweza kukabiliana na matatizo ya kiusalama na miundombinu. Tathmini hii imetangazwa kufuatia ziara ya Ujumbe wa Wafadhili wa Kongo unaoongozwa na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bruno Lemarqui katika jimbo hilo ili kutathmini hali ya mambo na kuhakikisha maendeleo na utulivu pale MONUSCO itakapoondoka. Ujumbe huu unaundwa na washirika yapata ishirini wa kiufundi na kifedha wa Kongo wakiwemo wakuu wa ushirikiano kati ya Kongo na nchi mbalimbali, wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, MONUSCO na mashirika na taasisi za Umoja wa Mataifa, ambayo kwa pamoja wanaunda kile kinachoitwa "Kundi la Uratibu wa Washirika".

Nchini Kenya, kamati ya bunge kuhusu masuala ya mambo ya nje imeanzisha vikao vya hadhara kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya mamlaka, vitendo vilivyofanywa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi yao ya mazoezi katika eneo la Nanyuki umbali wa Kilomita 180 kutoka jijini kuu Nairobi. Vikao hivyo vinavyofanyika eneo la Nanyuki, Laikipia na Samburu, vinafanyika baada ya tukio la mauaji ya mwanamke kwa jina Agnes Wanjiru yaliyoibua mjadala kimataifa. Kamati hiyo ya bunge imesema itachunguza makosa mengine kama vile unyanyasaji, matumizi mabaya ya mamlaka, ubaguzi na mienendo isiyokubalika.

Katika michezo...
Ilikuwa wikendi ya mishangao katika Ligi kuu ya Raga nchini, timu zote ambazo ziko katika nafasi ya chini katika ligi zilishinda mechi yazo. Baadhi ya wachezaji walikosekana katika timu nyingi kwa sababu yakuwa katika timu za State of Origin, mechi ya kwanza ya wanaume ikitarajiwa kuchezwa jioni ya Jumatano katika uwanja wa Sydney Olympic Park.
North Queensland Cowboys waliwashinda Sydney Roosters kwa alama mbili katika mechi ya mwisho ya raundi, wakati nahodha wa Roosters James Tedesco alikosa mechi hiyo baada yakuitwa kujiunga na kambi ya Blues wa NSW.

Share