Waathirika wa uhalifu wa vijana wanajiandaa kufanya maandamano mbele ya bunge la Queensland leo asubuhi [[30/4/24]], kuomba hatua ya moja kwa moja kutoka serikali ya jimbo. Trudy Reading anatoka katika kundi la Voice for Victims, wanao shiriki katika maandamano hayo. Ali eleza shirika la habari la Channel Nine kuwa wakaazi wa Queensland hawaku dhani bado watakuwa katika hali hiyo miezi tisa baada ya mwanzo wa misururu ya visa vya uhalifu wa vijana.
Zaidi ya watu 130,000 wame hamishwa na mafuriko nchini Kenya wakati idadi ya vifo ina endelea kuongezeka tena baada ya bwawa kuvunjika Jumatatu. Idadi mpya ya vifo kupitia mvua nzito na mafuriko tangu mwezi ulio pita, imefika watu 140 wakati maelfu zaidi wame hamishwa na mafuriko katika nchi zingine za Afrika Mashariki. Msemaji kutoka serikali ya Kenya amekana madai kuwa mamia ya watu wamefariki na amesema takwimu rasmi ya vifo kufikia Jumamosi 27 Aprili 2024 ilikuwa watu 76.
Umoja wa Ulaya umesema unaweka mchakato mgumu zaidi wa kupata visa kwa raia wa Ethiopia. Hatua hiyo inafuatia kile umoja huo imekitaja kuwa ukosefu wa "ushirikiano wa kutosha" katika kuwarudisha nyumbani waomba hifadhi waliokataliwa pamoja na wahamiaji. Hatua hiyo inamaanisha Waethiopia hawatatumia tena aina ya nyaraka wanazotoa ili kukidhi mahitaji ya maombi ya safari barani Ulaya. Hawawezi tena kupata visa ya kuingia Ulaya mara nyingi, na wanadiplomasia sasa watalazimika kulipa ada ili kupata visa.
Mahakama kuu nchini Ghana imefuta mashitaka kwa Rais Nana Akufo-Addo ya kushindwa kuchukua hatua za haraka kuhusiana na mswaada unaopinga Ushoga (LGBTQ) iliyopitishwa na Bunge mwezi Februari, ilitua hukumu hiyo Jumatatu. Wabunge ambao kwa idadi kubwa walipititisha sheria ambayo itaongeza ufuatiliaji wa haki za mashoga katika taifa hilo la Afrika Magharibi wamekuwa wakimtaka Akufo-Addo atangaze sheria hiyo mpya. Lakini ofisi ya rais imesema hautaupeleka mswaada huo kwa rais kuidhinishwa mpaka mashitaka hayo mawili dhidi yasuluhishwe, yamezua ukosoaji bungeni.
Mawaziri wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiwemo wa Fedha, na waziri wa zamani walipigwa marufuku wikiendi hii kuondoka nchini DRC na mahakama inayochunguza tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma. Hawa ni Mawaziri wa Fedha na Maendeleo ya Vijijini, Nicolas Kazadi na François Rubota mtawalia, pamoja na Waziri wa zamani wa Maendeleo ya Vijijini, Guy Mikulu. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Nicolas Kazadi, alipigwa marufuku siku ya Jumamosi kuondoka Kinshasa kuelekea Ufaransa, ambako Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, yuko katika ziara rasmi Jumatatu na Jumanne.