Taarifa ya Habari 30 Januari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wa Australia wame hakikishiwa hapatakuwa mageuzi yatakayo fanywa kwa faida ya kodi ya mwekezaji wa nyumba, hii ni baada ya mageuzi ambayo yalikuwa hayajatarajiwa kwa awamu ya tatu ya makato ya kodi.


Mlinzi wa watumiaji wa Australia amesema serikali inastahili ingilia kati sekta ya malezi ya watoto, ili kuifanya iwe nafuu zaidi, pamoja nakutaja nakuaibisha makampuni yanayo lipisha hela nyingi zaidi. Ripoti ya mwisho ya tume ya ushindani na wateja ya Australia kwa sekta hiyo, baada ya uchunguzi wa mwaka mzima imebaini kuwa ada za malezi ya watoto zime ongezeka haraka kuliko mfumuko wa bei.

Uchunguzi wa shirikisho umebaini kuwa "hata tisho dogo" kwa ushindani katika sekta ya usafiri wa anga, ina weza saidia kupunguza bei za tiketi kwa wateja. Matokeo ya mapema kutoka kwa uchunguzi wa ushindani, yame onesha kuwa wasafiri wa anga wanaweza tarajia kulipa nusu ya bei ya nauli ya tiketi kwa safari ambayo kuna kampuni tatu za ndege kulinganisha na sehemu kwenye kampuni moja.

Mataifa ya Afrika Magharibi ya Mali, Burkina Faso na Niger yamejiondoa kwenye shirika la kiuchumi la kieneo la ECOWAS, viongozi wao wa kijeshi wamesema Jumapili. Viongozi wa kijeshi wa mataifa hayo kupitia taarifa ya pamoja iliyosomwa kupitia televisheni zao zote za kitaifa, wamesema kwamba,” wamemua kupitia utaifa wao kamilili kujiondoa mara moja kwa Burkina Faso, Mali na Niger kuondoka ECOWAS, “ wakidai kuwa shirika hilo limeondoka kwenye malengo ya waanzilishi wake pamoja na wanaharakati wa Umoja wa Afrika, baada ya kuwepo kwa karibu miaka 50 tangu kubuniwa.

Licha ya kwamba shule zote nchini Kenya zimefunguliwa, maafisa wa elimu wanasema kuwa siyo kila mwanafunzi, aliyefikia umri wa kwenda kwa shule ya upili, amefanikiwa kuingia darasani. Mitandao ya kijamii nchini Kenya imejaa picha za wahitimu wa shule za msingi, wakiwa na mabango ya kuwaomba wahisani kuwasaidia karo ya shule ili waendelee na masomo.

Chama tawala nchini Afrika Kusini Jumatatu kimemisimamisha kwenye chama rais wa zamani Jacob Zuma na kuapa kuwasilisha mashtaka dhidi ya kundi pinzani linalofanya kampeni kwa jina lake. Akitangaza uamuzi huo, katibu mkuu wa ANC Fikile Mbalula amesema” Zuma na wengine ambao mwenendo wao unakinzana na maadili na kanuni zetu, watajikuta nje ya chama cha African National Congress.” Mwezi Disemba, alitangaza kwamba atafanya kampeni kwa niaba ya chama kipya, uMkhonto We Sizwe (MK) au mkuki wa taifa, jina la tawi la kijeshi la chama cha ANC wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.







Share