Waziri wa uhamiaji Andrew Giles amesema amefuta viza za wageni nane. Hali hiyo imejiri wakati Bw Giles amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa upinzani ambao unataka afutwe kazi. Anazingatia kujaribu kuwafukuza watu 30 baada ya mahakama ya rufaa kuwaruhusu wabaki Australia kwa misingi ya amri ambayo waziri mwenyewe alikuwa ametia saini.
Kulingana na kielezo cha hivi karibuni cha wahamiaji wa mikoani, vijana wana ongoza wanao hama kutoka miji mikuu wakielekea mikoani, wakiendeleza mtindo ulioanza wakati wa vizuizi vya janga la Uviko-19 na ime chochewa na gharama za maisha na kodi ya juu ya nyumba. Kieleza cha taasisi ya mikoa ya Australia, imetumia data kutoka benki ya Commonwealth, kutambua ukuaji wa mtindo huo pamoja nakupanga kwa uwekezaji wa miundombinu katika sehemu za kanda/mikoa. Watu wanao ondoka mijini hawa endi mbali ila, wanaenda katika mikoa ya karibu inayo jumuisha sehemu tano maarufu zakuhamia.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Afrika Kusini huku matokeo ya awali kutoka baadhi ya maeneo ya taifa hilo yakionyesha chama African National Congress, ANC kupoteza wingi wa viti bungeni. Matokeo ambayo yanaweza kuwa mabadiliko makubwa ya kisiasa tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi. Kulingana na takwimu za tume ya uchaguzi, kufikia sasa asilimia 11.3 ya kura zimeshahesabiwa, na chama cha ANC kimepata asilimia 42.8 ikifuatiwa na chama cha kileberali cha Democratic Alliance kwa asilimia 26.5 ya kura huku chama cha mwanasiasa Julius Malema cha Economic Freedom Fighters EFF kikichukua nafasi ya tatu kwa asilimia 8.3.
Muungano wa wanahabari wa Forbidden Stories umechapisha uchunguzi wake "Rwanda Classified" siku ya Jumanne, Mei 28, kuhusu ukandamizaji uliofanywa na mamlaka ya Rwanda dhidi ya wapinzani wa utawala wa Rais Paul Kagame, pamoja na waandishi wa habari wakosoaji. Taarifa kutoka kwa waandishi wa habari 50 kutoka nchi 11 tofauti zinafichua vitisho au majaribio ya mauaji ili kuzima sauti zote za ukosoaji, iwe nchini Rwanda au nje ya nchi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Burundi, Alain-Guillaume Bunyoni, amefika mahakamani kukata rufa kuhusu mashtaka anayokabiliwa nayo ikiwemo kujaribu kuipindua serikali, chanzo kutoka mahakamani kimethibitisha. Bunyoni alihudumu katika wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Burundi kuanzia katikati ya mwaka wa 2020 hadi mwezi Septemba mwaka wa 2022 ambapo alifutwa kazi baada ya rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu kuwepo kwa njama ya kuiangusha serikali yake. Alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi Desemba kwa madai ya kupanga njama ya kuangusha utawala uliochaguliwa kidemokrasia pamoja na kutumia uchawi kutishia maisha ya rais. Alikabiliwa pia na mashtaka ya kuhujumu usalama wa kitaifa, kuyumbisha uchumi sawa na makosa mengine.