Taarifa ya Habari 4 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho inakana ukosefu wa ukuaji wa tija kwa zamu yake ambayo imewagharimu wafanyakazi wapato la chini nyongeza yajuu zaidi ya mshahara. Tume ya Haki ya Kazi ime inua kima cha chini cha mishahara na tuzo kwa asilimia 3.75 itakayo anza Julai 1


Kama sehemu ya uamuzi wa kima cha chini cha mapato, Tume ya Haki ya Kazi imetangaza hivi karibuni ita zindua taratibu zakushughulikia kutothaminiwa kwa jinsia kwa tuzo za kisasa na uanishiaji unao tumiwa katika kazi zinazo tawaliwa na wafanyakazi wa kike. Hii ina maana ongezeko ya mishahara inaweza kuja katika sekta kama elimu ya mapema ya watoto, wafanyakazi wa malezi, wafanyakazi wa jamii, wanasaikolojia na wasaidizi wa madaktari wa meno.

Waziri wa uhamiaji Andrew Giles amesisitiza sehemu ambako wafungwa wa uhamiaji walio achiwa huru na hukumu ya mahakama kuu Novemba mwaka jana daina inajulikana, na usalama wa jamii hauja hatarishwa. Hiyo ni licha ya Bw Giles kulazimika kukanusha madai aliyotoa wiki iliyopita kuwa, ndege zisizo na rubani zinatumiwa kuwafuatilia wafungwa hao. Ame eleza bunge la shirikisho alipewa taarifa potofu na idara yake.

Ukulima wa Australia, uvuvi na uzalishaji wa misitu vinatarajia kurekodi mazao yao ya tatu makuu baada ya mafanikio ya msimu wa majira ya baridi na kuboresha mtazamano wa msimu. Taarifa hiyo nzuri inafuata mazingira ya ukame katika miaka iliyopita na inatarajiwa kuona sekta ikikuwa kwa thamani kwa $89.5 bilioni katika mwaka wa fedha ujao.

Randi ya Afrika Kusini imeimarika kwa kiasi mapema leo Jumatatu, huku wachambuzi wakisema wanatarajia kwamba mazungumzo ya kisiasa wiki hii, kuunda serikali yatachochea zaidi thamani ya sarafu hiyo. Hii ni baada ya chama tawala cha African National Congress ANC kushindwa kupata idadi ya viti vya bunge vinavyohitajika katika utawala wake wa miaka 30. Chama cha ANC kilipata asilimia 40.2 ya kura, ikiwa ni matokeo mabaya zaidi kuwahi kurekodiwa na chama hicho, na kitalazimika kufanya mazungumo na vyama vingine ili kuunda serikali. Wawekezaji wana wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa ANC kuhusisha vyama kama EFF cha Julius Malema au uMkhonto we Sizwe cha rais wa zamani Jacob Zuma, na wangependelea ANC kifanye mazungumzo na Democratic Alliance chenye sera za kibiashara.

Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Nigeria imesema kwamba mitambo yako imezima baada ya wafanyakazi kuanza mgomo. Muungano mkubwa wa vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria ilitangaza mgomo kuanzia leo Jumatatu, baada ya kushindwa kukubaliana na serikali kuhusu kiwango cha chini cha malipo kinachostahili kutolewa kwa wafanyakazi. Nigeria labour congress NLC na Trade union congress TUC vilitangaza mnamo Mei tarehe 1 kwamba wanachama wake wataanza mgomo iwapo makubaliano kuhusu kiwango cha chini cha mshahara yatakuwa hayajafikiwa kufikia mwishoni mwa mwezi.

Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo. Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika. Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia. Kongamano linafanyika wiki hii. Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Share