Upinzani wa shirikisho unaishtumu serikali kwakujaribu kushawishi mwamuzi huru wa ajira, baada yaserikali kutoa onyo kwa mipango yakujaribu kupunguza mamlaka ya waajiri kufuta mikataba ya kazi. Hata hivyo, waziri Brendan O'Connor ametupilia mbali madai ya upinzani.
Mashauriano juu ya mamlaka ya mikataba na kanuni za mapambano zinachelewesha kupelekwa kwa wanajeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chini ya jeshi la dharura la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Gazeti la The East Africa linafahamu kuwa nchi tano kati ya sita wanachama wa EAC – ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda na Sudan Kusini – ziko tayari kupeleka majeshi huko mashariki mwa DRC lakini zimesisitiza kuwepo kwa kanuni sahihi ili kuepuka makosa yaliyotokea katika vikosi vya awali vya kulinda amani.
Wakenya ndani na nje ya nchi waendelea kusubiri kujua kama uchaguzi wa urais utarudiwa au ushindi wa Dr William Ruto utaidhinishwa. Baada ya wiki nzima ya kila upande kutoa maombi na mawasilisho mbele ya majaji saba wa mahakama ya upeo, ngoja ngoja ya siku 14 sasa itafika tamati kesho ,Jumatatu tarehe 5.