Taarifa ya Habari 5 Disemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Get the SBS Audio app

Other ways to listen


Published

Updated

By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Serikali ya shirikisho inatarajiwa kuwasilisha mageuzi ya muswada wiki hii, kwa ajili yaku kabiliana na utata ambao ume ibuka baada ya uamuzi wa mahakama kuu ambayo ili toa hukumu kuwa kifungo ndani ya vizuizi vya uhamiaji ni kinyume ya sheria.


Waziri wa kigeni Penny Wong na mwenzake kutoka Ufararansa Catherine Colonna, wametangaza makubaliano mapya ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili, katik hatua yakuweka upya mahusiano kati ya Ufaransa na Australia.

Makubaliano hayo yana ipa jeshi la kila nchi ufikiaji katika vifaa vya washirika wake na, wame toa ahadi za ushirikiano zaidi katika shughuli kati ya majeshi husika.

Mnamo septemba 2021, serikali ya Waziri Mkuu Scott Morrison ilifanya maamuzi yakushangaza, kwa kujiondoa katika mkataba wa manowari wenye thamani ya dola bilioni 90 na Ufaransa, kwa ajili yakujiunga katika muungano wa AUKUS kati ya Marekani na Uingereza.

Waziri wa huduma za jamii Amanda Rishworth amejibu wito kutoka kwa mchunguzi wa jumuiya yamadola kuzingatia kusamehe takriban deni laki moja za Centrelink, kwa sababu ya hesabu zenye makosa.

Mchunguzi huyo alipata kuwa kuna uwezekano madeni hayo yote yamadola, yalipatikana kimakosa na Services Australia pamoja na idara ya huduma za jamii kati ya miaka ya 2003 na 2020.

Share