Taarifa ya Habari 6 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu amekosoa upinzani kwa kufeli kuwa na msimamo kwa pendekezo lake la awamu ya tatu ya makato ya kodi, wakati vikao vya bunge la shirikisho vina anza tena.


Serikali ya Queensland ime ahidi kujenga nakupata zaidi ya nyumba elfu 53,500 za jamii kufikia mwaka wa 2046. Kingozi wa Queensland Steven Miles amesema mfumo huo wa $1.25 bilioni ni geuzi jipya la serikali yake kwa mpango wa muda mrefu wa nyumba wakati janga la gharama ya maisha lina endelea.

Serikali ya shirikisho ime achia mpango wayo wa rasimu kwa vigezo vya ufanisi wa petroli, yenye lengo lakupunguza idadi ya gari mpya za wasafiri za uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 60 kwa muda wa miaka miaka mitano.

Wabunge nchini Senegal siku ya Jumatatu walianza kujadili pendekezo la kuahirisha uchaguzi wa rais, ambao hapo awali ulipangwa kufanyika Februari 25.

Rais wa Poland Andrzej Duda akiwa kwenye ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya ameahidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zao mbili. Rais Ruto kwa upande wake ametoa wito kwa wawekezaji wa Poland kutumia fursa zilizopo Kenya na mhimili wa uhusiano ulowekwa kama wito kwao kuinua faida ya nafasi ya Kenya kwa uwekezaji wao wa kikanda na barani Afrika.

Hofu inaongezeka katika baadhi ya maeneo katika wilaya ya masisi huko kivu kaskazini, baada ya waasi wa M23 kutangaza mwishoni mwa wiki kwamba wameudhibiti mji mdogo wa Shasha unaoiunganisha miji ya Goma na Bukavu.

Share