Serikali haijaweka wazi idadi ya wafungwa wakigeni ambao wanaweza rejeshwa gerezani chini ya sheria mpya, zilizo undwa nakupitishwa bungeni jana jumatano. Mwanaume mwenye miaka 45 ni amekuwa mfungwa wazamani wa nne ambaye amefunguliwa mashtaka mapya baada yakushtumiwa kwa kuvunja amri ya kutotoka nje kwa masharti ya viza yake nakuiba mizigo katika uwanja wa ndege wa Melbourne.
Tathmini mpya ya mfumo wa kitaifa wa bima ya ulemavu, imepata mfumo wa msaada wa walemavu wa Australia, unategemea sana mfumo, kusababisha uchaguzi wa udhibiti mdogo kwa watumiaji. Ripoti hiyo huru, iliyo achiwa leo ili agizwa na serikali kutazama ufanisi endelevu wa mifumo, wakati gharama inaendelea kuongezeka kwa kiwango kisicho endelevu cha 14% kwa mwaka. Tathmini hiyo ilipata kuwa serikali inategemea sana, NDIS kama mfumo wa pekee wa msaada kwa watu wanao ishi na ulemavu na, imependekeza kuundwa kwa misaada yakimsingi inayo weza tolewa kwa wa Australia wote wenye ulemavu bila kujali kama wako katika mfumo wa NDIS.
Kimbunga cha tropiki Jasper, kimeongezwa kuwa kiwango cha tatu na kinatarajiwa kuongezeka nguvu zaidi kinapo elekea katika pwani ya Queensland. Kimbunga Jasper kimetabiriwa kufikia kiwango cha 4 kwa ukali kufikia leo Alhamisi na kuna uwezekano kufika usiku wa Alhamisi kinaweza kuwa katika kiwango cha 5, kwa mujibu wa utabiri mpya kutoka ofisi ya utabiri wa hewa.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amekitaka chama chake cha kihafidhina kiuunge mkono mpango wake wa kuwapeleka wakimbizi nchini Rwanda na kuhimiza mkazo zaidi ili mpango huo usisambaratike.
Sunak amesisitiza kuwa mpango wake juu ya wahamiaji unafanya kazi, wakati ambapo suala hilo linatishia kukigawa chama cha Conservative. Waziri mkuu huyo anakabiliwa na changamoto kubwa kabisa tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita wakati anapofanya juhudi za wabunge wenye mrengo wa kulia wanaotaka Uingereza ijiondoe kwenye mikataba ya kimataifa, ili iweze kuweka sera yake ya uhamiaji.
Waziri wake wa masuala ya uhamiaji Robert Jenrick alijiuzulu hapo jana, na sasa Sunak anakabiliwa na maswali, iwapo ataweza kuitekeleza sera yake kwa kupitia njia ya kura ya bungeni.
Marekani imesema jana kwamba majeshi pinzani nchini Sudan kwa pamoja yamefanya uhalifu wa kivita katika mzozo baina yao. Washington aidha imedai kuwepo kwa kampeni ya safishasafisha ya kikabila katika jimbo la Darfur,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasilisha ripoti hiyo iliyotokana na uchunguzi uliofanywa na wizara yake, baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka wasiwasi na mazungumzo kushindwa kutoa suluhu.
Katika taarifa za michezo, Kiongozi wa shirika la mchezo wa Rugby Australia Phil Waugh, amesema bila shaka mlango uko wazi kwa Mark Nawaqanitawase kuendelea kuchezea timu ya taifa ya raga katika mwaka wa 2024, licha ya mchezaji huyo kuthibitisha anahamiaa katika mchezo wa NRL.
Nawaqanitawase, ambaye amechezea Australia mara 11 tangu alipo cheza mechi yake ya kwanza yakimataifa katika ziara ya Ulaya, ata jiunga na timu ya Sydney Roosters kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia 2025.
Hatua hiyo ya moja wa nyota mkubwa wa mchezo wa raga, ni igo kubwa kwa shirika la Rugby Australia, katika wakati ambapo mchezo huo uko chini ya shinikizo kubwa baada ya kampeni yakusikitisha ya kombe la dunia.
Rugby Aaustralia bado haija amua mwalimu atakaye rithi mikoba ya Eddie Jones, ila, miongoni mwa vitu vya kwanza vya kufanya vya mwalimu mpya, itakuwa jinsi yaku kabiliana na hatua ya Nawaqanitawase katika mwaka wa 2024.