Taarifa ya Habari 7 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri wa serikali ya shirikisho Bill Shorten amesema hawezi sema kama chama cha Labor kita weka chama cha Greens mwisho, katika kadi zao za maelezo ya jinsi yakupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu ya msimamo wa chama cha Greens kwa mgogoro wa Gaza.


Vyama vya Labor na upinzani wa mseto vili kikosoa chama cha Greens wiki iliyopita, vikisema chama hicho kina chochea mivutano ndani ya jamii nchini Australia kwa sababu ya mgogoro wa Gaza. Kwa upande wake kiongozi wa shirikisho wa chama cha Greens Adam Bandt alijibu ukosoaji huo akikemea vurugu ya aina yoyote. Ametishia kumfungulia mashataka mwanasheria mkuu wa taifa Mark Dreyfus kwa madai ambayo Bw Dreyfus alitoa kumuhusu katika mahojiano aliyofanya na shirika la habari la ABC. Bw Shorten ali eleza shirika la habari la Network kuwa chama cha Greens haki jiendeshi katika hali inayo faa kitaalam.

Vyama vya wafanyakazi vinaomba mishahara ya vijana ifutwe na vijana ambao ni wafanyakazi walipwe sawia na wafanyakazi wenza ambao ni watu wazima. Katika baadhi ya sekta, wafanyakazi ambao ni vijana wanaweza lipwa chini ya asilimia 50 ya mshahara, kulinganishwa na watu wazima licha ya kiwango cha kazi wanayo fanya. Kuongezea, wanaweza lipwa malipo ya ustaafu tu, kama wame ajiriwa kufanya kazi zaidi ya masaa 30 kila wiki. Baraza la vyama vya wafanyakazi wa Australia (ACTU) limekubali kumaliza ubaguzi wa umri na hatua zingine kwa upendeleo wa wafanyakazi ambao ni vijana.

Waziri wa uhamiaji Andrew Giles ametia saini mwelekeo mpya wa uwaziri unao hitaji mahakama ya rufaa ya utawala, izingatie usalama wa jumuiya wakati inafanya tathmini ya maaumizi ya kufutwa kwa viza. Mwelekeo huo mpya unao julikana kama Mwelekeo wa Uwaziri 110, uta anza kutumika katika wiki mbili zijazo na, unahitaji AAT kuchukua njia ya akili ya kawaida kwa kesi na kuweka uzito zaidi kwa usalama wa jamii pamoja na maswala ya vurugu yakifamilia na jinsia.

Maeneo ya kusini na kusini magharibi ya Sydney, yana onywa yafanye tahadhari kuhusu mafuriko leo Ijumaa 7 Juni, wakati jimbo la New South Wales lina endelea kukumbwa kwa mvuo nzito. Barabara kuu ya Picton, kusini magharibi mwa Sydney inatarajiwa kufurikwa.
Mafuriko ya wastan yanatarajiwa katika maeneo ya Colo, Nepean, na Hawkesbury Rivers ambayo yake kusini-magharibi mwa Sydney, na mito ya Georges na Woronora katika eneo la kusini ya mji huo. Shirika la huduma ya dharura ya jimbo hilo, limefanya uokoaji 49 wa mafuriko hadi sasa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekuwa akikutana na maafisa wakuu wa chama cha African National Congress siku ya Alhamisi ili kuamua jinsi ya kuunda serikali baada ya chama hicho kupoteza utawala wake wa miaka 30 na kuwa katika mkwamo baada ya uchaguzi. ANC imeonyesha kuegemea upande wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itavileta pamoja vyama vingi vya siasa katika makubaliano mapana, badala ya muungano wa moja kwa moja na upinzani mkuu, Democratic Alliance, au DA.

Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo. Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika. Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Wizara ya afya nchini Kenya imepokea zaidi ya dozi milioni 8 za chanjo za msingi za watoto baada ya uhaba kuripotiwa kote nchini. Kwa mujibu wa katibu wa huduma za afya, Harry Kimtai, wizara ya afya inajitahidi kufikisha chanjo hizo kwenye hospitali za umma ifikapo mwishoni mwa wiki ya pili ya mwezi huu wa Juni. Shehena hiyo inajumuisha dozi milioni 1.2 za chanjo ya ukambi, milioni tatu za chanjo ya maji ya Polio, milioni moja ya Pepopunda na milioni tatu za Kifua Kikuu. Shehena hii ya chanjo imepatikana kupitia jumuiya ya wafadhili na watengezaji wa chanjo, GAVI.

Watu zaidi ya 15 wameuawa mashariki mwa nchi ya DRC, baada ya wapiganaji wa ADF wenye uhusiano na kundi la kiislamu la Islamic State kutekeleza mashambulio kwenye vijiji kadhaa ambapo walichoma moto nyumba na kuwachinja raia. Waasi hao wamezidisha mashambulio katika siku za hivi karibuni, huku FARDC likishirikiana na jeshi la Uganda likitarajia kuhamishia operesheni zake matika maeneo hayo.

Share