Taarifa ya Habari 8 Aprili 2024

City - Swahili.jpg

Kiongozi wa chama cha Nationals David Littleproud amesema anaunga mkono adhabu kwa tabia mbaya za maduka makubwa ila, ameongezea kuwa mabadiliko hayo hayata jiri haraka yakutosha kwa watumiaji.


Leo hii Aprili 7 serikali ya Albanese, ilitoa ripoti ya muda ya waziri wa ushindindani wa zamani wa Labor Craig Emerson, kuhusu msimbo wa chakula na mboga. Mapendekezo ya Dr Emerson yana jumuisha kufanya mpango wa hiari kuwa lazima, kuipa tume ya ushindani na watumiaji ya Australia, mamlaka yakulazimisha adhabu zilizo pendekezwa kufika hadi dola milioni 10. Hata hivyo, Waziri Mkuu haja unga mkono wito wa pamoja kutoka vyama vya shirikisho vha Nationals na Greens, kuvunja maduka mawili makubwa nchini ya Woolworths na Coles.

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema Australia inataka "majibu sahihi" kwa shambulizi la Israeli lililo uwa mfanyakazi wa mashirika ya msaada kutoka Australia Zomi Franckom. Kiongozi wa zamani wa jeshi la Australia Mark Binskin, ameteuliwa kuwa mshauri maalum wa serikali ya shirikisho kwa jibu la Israel kwa shambulizi hilo la Aprili mosi, ambalo lili wauwa wafanyakazi saba wa shirika la World Central Kitchen mjini Gaza. Mkuu wa Jeshi la Anga mstaafu Binskin anatarajiwa kutoa ushauri kwa maswala yanayo jumuisha mipangilio kwa uchunguzi huru, sera za Jeshi la Israel, taratibu za matukio ya uendeshaji pamoja na taratibu zakuwajibisha walio husika.

Wakaaji wa maeneo ya kaskazini magharibi Sydney, wanarejea nyumbani mwao baada ya maji ya mafuriko kutoka dhoruba ya Ijumaa kupungua, na amri zaku ondoka katika makaazi yao kuondolewa. Zaidi ys nyumba 60, zimeripotiwa kuwa zimeharibika, wakati nyumba 17 kati yazo hazimo katika hali inayo ruhusu watu waishi ndani katika kanda ya Sydney. Uongozi wa Jimbo hilo umetangaza baadhi ya maeneo ya kanda kuwa ni maeneo ya maafa ya asili, ili maeneo hayo yaweze pata misaada kwa wanao ihitaji.

Zaidi ya watu 90 walifariki wakati boti iliyojaa watu wengi ilipozama katika pwani ya kaskazini mwa Msumbiji, mamlaka za eneo hilo zilisema Jumapili. Boti hiyo iliyokuwa ya uvuvi ilikuwa imebeba watu 130, ilipata matatizo ilipojaribu kufika kwenye kisiwa kilicho karibu na mkoa wa Nampula, maafisa walisema.
“Kwa sababu boti hiyo ilikuwa imejaa watu wengi na haikufaa kubeba abiria iliishia kuzama. Kuna watu 91 waliofariki,” alisema katibu wa mkoa wa Nampula Jaime Neto. Aliongeza kuwa watoto wengi ni miongoni mwa waliokufa.

Rwanda jana Jumapili 07.04.2024 ilitimiza miaka 30 tangu yafanyike mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya walio wachache ya Watutsi. Wahutu waliowasaidia Watutsi pia waliuawa manmo mwaka 1994. Rais wa Rwanda Paul Kagame aliwasha mwenge, hio ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji hayo katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari katika mji wa Kigali. Mauaji hayo yalitokea Aprili 7 mwaka 1994 ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wanaaminika walizikwa katika eneo hilo.

Katika michezo:
Wa Australia Tim David na Marcus Stoinis wamesaidia timu zao kupata ushindi katika ligi kuu ya kriket ya India. David alipata mikimbio 45 kutoka kwa mipira 22 na kuisaidia timu yake ya Mumbai Indians, kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Delhi Capitals Jumapili 7 Aprili 2024.

Share