Taarifa ya Habari 8 Februari 2024

City - Swahili.jpg

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape, ame hotubia bunge la Australia.


Katika hotuba ya kwanza ya bungeni kutoka kwa kiongozi wa mataifa ya visiwa vya Pasifiki, Bw Marape alitambua historia inayo changiwa na mataifa hayo mawili wakati akitazamia ushirikiano wa siku za usoni. Papua New Guinea ilipata uhuru kutoka Australia mnamo mwaka wa 1975.

Muswada wa serikali ya Labor wa mahusiano ya viwanda, unatarajiwa kupitishwa bungeni leo. Muswada huo wakuziba mapengo, unafafanua upwa maana ya kuajiriwa kwa muda pamoja nakuwasilisha viwango vya chini kwa wafanyakazi wa maukio.

Haki yakukata muunganisho, inayo wazuia waajiriwa kuto adhibiwa kwa kupuuza mawasiliano ya kazi wanapokuwa katika wakati wao binafsi, imeongezwa katika muswada huo kwa ajili yakuungwa mkono na wabunge huru pamoja na chama cha Greens.

Zaidi ya wafanyakazi 1000 wame susia kazi kwa muda wa masaa 24, kwa sababu ya mgogoro wa mshahara katika makampuni mawili makubwa ya pwani ya kaskazini ya umeme. Chama cha wafanyakazi wa umeme kina pambana na makampuni mawili makubwa ya umeme ya Transgrid na Endeavour Energy. Chama hicho kina taka ongezeko la 8% kwa mishahara kwa muda wa miaka mitatu na kina dai mishara katika kampuni ya Endeavour imeongezeka kwa 10.5% tangu 2019 na 8% katika kampuni ya Transgrid, wakati mfumuko wa bei umefika 18% katika wakati huo.

Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano umezitaka nchi kutowasahau raia waliojikuta katikati ya vita nchini Sudan, ikiomba dola bilioni 4.1 kukidhi mahitaji yao ya kibinadamu na kuwasaidia wale waliokimbilia nchi jirani. Miezi kumi ya vita huko Sudan kati ya vikosi vya jeshi na vya wanamgambo wa Msaada wa Dharura vimeharibu miundo mbinu ya nchi hiyo na kusababisha maonyo ya njaa na ukosefu wa makazi kwa mamilioni ya watu ndani na nje ya nchi. Nusu ya idadi ya watu wa Sudan- takriban watu milioni 25- wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi, wakati zaidi ya watu milioni 1.5 wamekimbilia Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chadi, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kufuatia visa vya mashambulizi yanayofanywa dhidi ya watu baada ya taarifa zao kukusanywa ama kuwasiliana na wahalifu mitandaoni, mamlaka nchini Kenya zinahimizwa kuchukuwa hatua za kuwalinda raia wake dhidi ya uhalifu.

Akisimulia tukio la mauaji ya mwanafunzi aliyehadaiwa mtandaoni, ambalo wamekuwa wakilifanyia uchunguzi, Kamisha wa Kaunti ya Nakuru, Lyford Kibaara, anasema ukosefu wa usalama kwa watoto na vijana kwenye mtandao ni hali inayotia wasiwasi. Visa vingi vya unyanyasaji mtandaoni vinachangiwa na upatikanaji rahisi wa maudhui ya picha za ngono, ulaghai wa mtandaoni na uingiliaji wa masuala ya faragha.

Katika taarifa za michezo, mchezaji wa South Sydney Rabittohs Tom Burgess anakaribia kustaafu baada yakutangaza kuwa msimu wa 2024 utakuwa msimu wake wa mwisho katika NRL na atahamia katika ligi ya Uingereza ya Super League. Mchezaji huyo mwenye miaka 31 ata jiunga na timu ya Huddersfield kutoka Souths, ambako ame tia saini mktaba wa miaka mitatu. Hatua hiyo ita hitimisha miaka 15 ya familia yake katika timu ya Rabbitohs, uhusiano huo uli anza kaka yake Sam alipo shawishiwa kujionga na timu hiyo ya Redfern na mmiliki wayo Russell Crowe mnamo 2010.                   

Share