Utafiti mpya wa watu wanao ishi na ulemavu umepata, wanapinga mapendekezo kadhaa ya utafiti wa hivi karibuni wa kikundi cha utetezi wa mpango wa taifa wa bima ya walemavu. Waziri wa mfumo wa bima ya ulemavu yakitaifa, Bill Shorten ali agiza uchunguzi huru wa mradi huo mnamo mwaka wa 2022, na mapendekezo 26 yanayo lenga kuwarejesha watu wenye ulemavu katika kitovu cha NDIS, kwa kurejesha imani katika mfumo huo.
Vipande vya kemikali ya Asbestos vilivyo patikana katika viwanja sita mjini Melbourne, vimelaumiwa kwa utupaji harama taka. Msimamizi wa maswala ya mazingira wa Victoria, ame amuru halmashauri moja ya jiji itoa ikabidhi mamlaka vitabu vyake vya kumbukumbu, pamoja nakuwaleta wataalam wafanye vipimo vya kina katika viwanja vya starehe baada ya asbestos kupatikana katika viwanja kadhaa mjini Melbourne mwezi huu.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba alikuwa na wasiwasi wa kile anachokiona kama kushindwa kwa Marekani kuyatambua mauaji ya Mauaji ya 1994 kama mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache nchini humo. Kagame amewaambia waandishi wa habari kwamba suala hilo lilikuwa ni "mada ya mazungumzo" walipokutana na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliyeongoza ujumbe wa Marekani nchini Rwanda kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji hayo.
Zaidi ya watu 90 walifariki wakati boti iliyojaa watu wengi ilipozama katika pwani ya kaskazini mwa Msumbiji, mamlaka za eneo hilo zilisema Jumapili. Boti hiyo iliyokuwa ya uvuvi ilikuwa imebeba watu 130, ilipata matatizo ilipojaribu kufika kwenye kisiwa kilicho karibu na mkoa wa Nampula, maafisa walisema.
Wakulima nchini Kenya waliopewa mbolea ghushi watafidiwa na serikali ya Kenya baada ya kampuni moja kutajwa kuwahadaa wakulima na hivyo kuiweka serikali katika hali ngumu kufuatia Sakata hilo. Aidha serikali Alisema itapunguza zaidi bei ya mbolea ili kuwanufaisha wakulima. Suala la Mbolea limekuwa moja ya suala kuu katika ajenda ya Rais William ruto hasa wakati wa kampeni ya mwaka 2022 kabla ya kupata ushindi.