Tetemeko la ardhi lenye vipimo vya 4.3 limetikisa mji wa Melbourne na maeneo kadhaa ya Victoria. Tetemeko hilo lili fanyika mida ya saa sita hamsini usiku, na kitovu chake kilikuwa karibu ya mji wa Leongatha ambao uko katika eneo la South Gippsland.
Binti ya bibi aliye chomwa kisu hadi kufa katika kituo cha ununuzi ameomba amani, baada ya ripoti za ukatili dhidi ya jamii zawa Afrika kuibuka. Vyleen White mwenye miaka 70, alichomwa kisu hadi kufa mbele ya mjukuu wake wa kake katika eneo la Redbank Plains ambalo liko Ipswich jumamosi Feburari 4 katika kisa cha wizi wa gari. Wavulana watano wenye umri kati ya miaka 15 na 16, wamefunguliwa mashtaka kwa tukio hilo na mwingine amefunguliwa shtaka la kuuwa.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitumia hotuba yake bungeni siku ya Alhamisi kuelezea mafanikio ya chama chake katika miaka 30 iliyopita, lakini akatoa maelezo machache kuhusu mipango yake ya kushughulikia changamoto kuu zinazoendelea kuikumba nchi hiyo.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema leo kuwa mataifa ya Niger, Mali na Burkina Faso yameshindwa kuheshimu sheria kwa kujiondoa katika kundi hilo.
Kufuatia mkasa wa mlipuko wa gesi eneo la Embakasi, mjini Nairobi mwishoni mwa wiki, miji mengine sasa inachukua tahadhari ili kuepusha maafa sawia na hayo siku za usoni.
Mjini Mombasa Gavana wa jimbo hilo Abdulswamad Sharrif Nassir ameamrisha kufungwa kwa maduka na vituo vya uuzaji gesi kinyume na sheria. Washukiwa wa kiwanda cha gesi cha Embakasi, Nairobi kilichosababisha vifo vya watu saba na mamia kujeruhiwa, wakiendelea kuzuiliwa na polisi, serikali ya jimbo la Mombasa , imefunga vituo vya biashara za gesi vinavyoendeshwa kinyume na sheria.