Tundu Lissu ashinda uchaguzi wa uongozi wa CHADEMA

Bw Tundu Lissu akitoa hotuba mbele ya wanachama wenza.jpg

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimetua kiongozi wake mpya kuelekea uchaguzi Mkuu wa urais wa mwezi Oktoba.


Freeman Mbowe, ambaye amekuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi cha miongo miwili, kupitia mtandao wake wa X zamani ukiitwa Twitter amempongeza mrithi wake na mkamu wake wa zamani Tundu Lissu kwa uteuzi wake.

Bw Freeman Mbowe akihotubia wanachama kabla ya uchaguzi wa kiongozi.jpg
Uteuzi wa Lissu unakuja wakati huu ambapo tofauti zikionekana kuibuka ndani ya chama hicho cha upizani, changamoto ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda ikikadhoofisha chama kuelekea uchaguzi Mkuu.

Aidha uchaguzi wa Chadema pia umefanyika wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na kipindi kigumu, wakosoaji wa serikali wakionekana kukabiliwa na serikali katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share