Ujuzi wa huduma ya kwanza unaweza okoa maisha, hivi ndivyo nasehemu yakupata mafunzo nchini Australia

wanafunzi washiriki katika masomo ya huduma ya kwanza ya CPR

wanafunzi washiriki katika masomo ya huduma ya kwanza ya CPR Source: Getty / Getty Images

Watu wengi huwa hawatarajii kuwa katika hali ya dharura, hadi wanapo jipata katika hali hiyo.


Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu ambao wamefanya mafunzo ya huduma ya kwanza nchini Australia, ni wachache sana wakilinganishwa na matukio ya majeraha yanayo hitaji majibu ya haraka.

Kwa hiyo, ni njia gani bora yakupata mafunzo?

Katika mwaka wa 2017, shirika la msalaba mwekundu lilipata kuwa Australia ina moja ya kiwango cha chini cha mafunzo ya huduma ya kwanza duniani, licha ya takriban nusu milioni ya watu wanao jeruhiwa huwa wana lazwa hospitalini kila mwaka. Miongoni mwa majeruhi kuna watoto elfu 60.

Makadirio ya shirika la Royal Life Saving Society yanadokeza kuwa, kwa wastan wa Australia 20 hufariki kupitia mishtuko ya moyo kila siku. Makadirio hayo yalipata pia kuwa 60% ya majeraha yanayo hitaji matibabu ya huduma ya kwanza hufanyiwa nyumbani.

Chini ya mwajiriwa mmoja kati ya watatu, wana amini kuwa wanaweza fanya huduma ya kwanza pakiwa dharura katika sehemu ya kazi.

Share