Ramadan na Eid ni nini na huwa zina adhimishwa aje nchini Australia?

Lantern With Moon Symbol And Mosque Shape Background. Ramadan Kareem And Islamic New Year Concept.

Photo taken in Bangkok, Thailand Credit: Songyuth Unkong / EyeEm/Getty Images

Je! ushawahi jiuliza umuhimu wa Ramadan na Eid ni nini katika utamaduni waki Islamu? Na sherehe hizi zina umuhimu gani kwa marafiki, majirani na watu unao fanyakazi nao ambao niwa Islamu?


Key Points
  • Ramadan is the holiest month in Islam during which healthy adult Muslims fast from dawn to dusk.
  • Eid al-Fitr is a three-day celebration of end of the holy month of fasting.
  • Muslim Australians bring their distinctive cultural practices to the celebration of Eid.
Australia ni nyumbani kwa zaidi ya idadi yawa Islamu 813,000, ambao ni sehemu ya idadi yawa Islamu bilioni 1.97 duniani.

Katika nchi yenye tamaduni nyingi kama Australia, inaweza kuwa vigumu kumpata mtu ambaye hajakutana, hajawa rafiki au kufanya kazi na mtu kutoka tamaduni au dini tofauti na lake.

Kuelewa nakuheshimu dini na tamaduni zawatu wengine, ni moja ya kipengele cha msingi cha jamii yenye mshikamano wakitamaduni.

Waislamu nchini Australia na sehemu zote duniani, hufanya mfungo wa Ramadan, ambao ni safari ya mwezi mzima ya ibada nakufunga.
Man praying in the sunset (Pixabay).jpg
The Islamic Hijri calendar, is based on the cycles of the moon around the Earth. Credit: Pixabay

Kwa hiyo, Ramadan ni nini?

Ramadan ni mwezi wa tisa wa kalenda yaki Islamu ya lunar, ambapo watuwazima ambao ni waislamu na wenye afya nzuri, wanatakiwa kufunga kuanzia alfajiri hadi jua linapo tua.

Zuleyha Keskin ni Profesa mshiriki na pia yey ni Kiongozi mshiriki wa Kituo cha masomo yaki Islamu na Ustaarabu katika chuo cha Charles Stuart mjini Melbourne.

Amesema mchakato mkubwa wakujifunza au maendeleo na nidhamu, hufanyika kwa Waislamu wakati wa mwezi wa Ramadan.
Ramadan is considered the holiest month of the year for Muslims and that makes it a very special month.
Associate Professor Zuleyha Keskin, Associate Head of the Centre for Islamic Studies and Civilisation at Charles Stuart University, Melbourne.
Kalenda yaki Islamu, inayo julikana pia kama kalenda ya Hijri, hutumia mizunguko ya mwezi kuzunguka dunia. Kwa sababu ni kati ya siku 10 hadi 12 kwa ufupi kuliko mwaka wa solar, tarehe kwa hafla zaki Islamu hutofautiana kila mwaka.

Mwaka huu, mwezi mtukufu wa Ramadan utakuwa kati ya 22 Machi na 20 Aprili 2023.
Shot of a young muslim woman pouring drinks for her family
A meal with loved ones during Ramadan. Source: iStockphoto / PeopleImages/Getty Images/iStockphoto

Kwa nini waislamu wanatakiwa?

Kufunga (Sawm katika Kiarabu) ni moja ya Nguzo Tano za Uislamu, ambazo ni: Taaluma ya Imani, kusali, kutoa sadaka, kufunga na kushiriki katika Hajj.

Wakati wakufunga haswa, waislamu wanatakiwa kujizuia kuvuta sigara, kujamiana, kuonesha hasira au kuhusika katika ubishi pamoja nakufanya matendo maovu.

Kwa kuongezea, ibada za ziada kama vile sala, kusoma nakuelewa Quran pamoja na kazi za hisani zina himizwa. Waislamu wengi pia hu hudhuria misikiti baada yakufuturu.

Profesa Karima Laachir ni Mkurugenzi wa Kituo cha masomo yawa Arabu na Uislamu katika chuo cha Australian National University, amesema Ramadan inahusu mengi zaidi yakujizuia kuto kula au kutumia vinywaji.

“Mhimu sana, ni mwezi wakiroho, ni mwezi unao tengwa kujiunga na imani ya mtu, Mungu,” Prof Laachir ali elezea.
It's a month where we re-learn to be compassionate human beings, to understand the needs of people who are poor, who cannot afford to eat and reconnect with the world around us.
Professor Karima Laachir, Centre for Arab and Islamic Studies, ANU
Mbali nakuwa aina ya maombi na wajibu wakidini, Profesa Laachir ameongezea kuwa, kuna faida pia kwa afya kupitia kufunga.

“Kimwili, ina manufaa kwa afya kwa sababu inasimamia mabadiliko ya seli yanayo fanyika ndani ya mwili, ina takasa sumu iliyo ndani ya mwili. Kwa hiyo imethibitishwa kuwa mchakato wa afya na tunajua kuhusu jinsi kufunga kwa vipindi ni mhimu kwa mwili.”
Friends gathering for eating dinner together
Healthy adult Muslims are required to fast from dawn to dusk during Ramadan. Source: Moment RF / Jasmin Merdan/Getty Images

Eid ni nini?

Na waislamu wanapo maliza mwezi wakufunga, Eid hufuata.

Eid ni neno laki arabu linalo maanisha ‘sherehe’ au ‘karamu’ na kuna Eid mbili katika kalenda yaki Islamu: Eid al-Fitr na Eid al-Adha.

Eid al-Fitr, hujulikana pia kama ‘Eid ndogo’, ni sherehe ambayo hudumu kwa siku tatu, ikiadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadan au kufunga.
Eid al-Fitr is an opportunity to celebrate what one has achieved during the month of Ramadan.
Dr Zuleyha Keskin, Centre for Islamic Studies and Civilisation, Charles Stuart University
Wanapo adhimisha Eid, Waislamu wanawajibu pia wakutoa sadaka, ambayo inajulikana kama Zakat al-Fitr, ili masikini nao waweze sherehekea.

Profesa Laachir ameongezea kuwa, Eid al-Fitr ni sherehe ya “kuwa pamoja na msamaha” kwa sababu ina fufua moyo wa jamii naku wahamasisha waislamu kuomba msamaha.

Zaidi ya hayo, inatoa fursa nzuri kwa watoto kuburudika, kupata marafiki wapya na kufahamu tamaduni yao.
Tradicionalni muslimanski roditelji i njihova djeca dijele lepinju tokom iftara u Ramazanu
In most Islamic countries, Eid al-Fitr is a public holiday. Source: iStockphoto / Drazen Zigic/Getty Images/iStockphoto
Kununua nguo mpya za watoto, kufanya usafi nyumbani, pamoja nakuandaa vitu vitamu maalum na vyakula, ni sehemu kubwa ya maandalizi ya Eid.

Mwaka huu Eid al-Fitr itakuwa 21 au 22 Aprili, kutegemea na wakati mwezi utaonekana. Katika nchi nyingi zaki Islamu, Eid al-Fitr ni likizo ya umma.

Kuhusu Eid al-Adha, ambayo hujulikana pia kama ‘Eid ya kafara’ au ‘Eid kubwa’, huwa ina sherehekewa baada ya hija ya kila mwaka, na huwa ina sherehekea nia ya Abrahamu kuheshimu amri ya Mungu, kumtoa kafara mwanawe Ishmael.
EID AL FITR  SYDNEY
Members of the Muslim community celebrate Eid al-Fitr, marking the end of the month-long fast of Ramadan with prayer at Lakemba Mosque in Sydney. Source: AAP / DEAN LEWINS/AAPIMAGE

Waislamu nchini Australia husherehekeaje Eid?

Sherehe za Eid al-Fitr huanza kwa sala maalum asubuhi ya siku ya kwanza ya mwezi wa kumi wa kalenda yaki Islamu.

Sala za jamii hufanywa katika misikiti ya vitongoji pamoja na ndani ya kumbi za jamii ambako watu, huamkiana wakisema ‘Eid Mubarak’.

Familia namarafiki hutembeleana na nikawaida kwa jamuia kuandaa sherehe za pamoja wakati wa Eid.

"Ni sherehe ya pamoja ya familia ambako, watu hutembeleana na, wanaburudika kwa siku tatu za sherehe za Eid al-Fitr, kupitia karamu na chakula, keki maalum na vyakula vingine," Prof Laachir aliongezea.

Hata hivyo, Waislamu wa Australia wanatoka katika nchi nyingi zenye tamaduni tofuati na sherehe zao pia zina tofautiana.
RAMADAN EID SYDNEY
Large crowds filled the Mosque in Lakemba and lined the streets to mark the end of the holy month of Ramadan, Sydney. Source: AAP / JANE DEMPSTER/AAPIMAGE
Ali Awan ni mu Australia mwenye asili ya Pakistan ambaye huwa na shughuli nyingi haswa wakati wa Eid al-Fitr kila mwaka. Yeye huwa ana anda moja ya sherehe kubwa zaidi yatamaduni nyingi ya Eid nchini Australia.

Amesema kuna tofauti "kubwa" zakitamaduni kati yawa Islamu kutoka mazingira tofauti. Kazi yake kama mwenyekiti wa sherehe za Eid za tamaduni nyingi ya Australia, niku waleta wote pamoja katika sehemu moja.

“Baadhi ya watu hupika vyakula tofauti na, wana mavazi tofauti ambayo huwa wana vaa katika siku ya Eid. Kisha, inapokuja kwa sherehe, inaweza kuwa kwa upande wa shughuli fulani, baadhi ya maonesho, baadhi ya njia za uchunguzi na vitu hivyo vyote,” Bw Awan ali fafanua.
During the Eid festival, we try to bring together all of the different performances, different cultures into one place and that’s the beauty of Australia.
Ali Awan, Australian Multicultural Eid Festival
Profesa Laachir anakubaliana naye, akiongezea kuwa sherehe za Eid nchini Australia, ni tofauti zaidi na zina nguvu kuliko katika nchi nyingi zaki Islamu.

“Uzuri wa jumuiya yawa Islamu wa Australia ni, sherehe nyingi hufanyika ndani ya vituo vya jamii na katika misikiti ya vitongoji, hali ambayo huleta pamoja jamii hizi, kutoka mazingira tofauti,” alisema.

Share