Taarifa ya Habari 3 Aprili 2025

Bench - Swahili.jpg

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema serikali ita toa dola milioni 50, kwa sekta zitakazo athiriwa kwa tangazo jipya la ushuru kutoka Marekani.


Mvua inatarajia kupungua katika maeneo ya ndani ya Queensland ila, tisho la mafuriko bado lina endelea kuwa. Sehemu za kusini magharibi Queensland zilipokea zaidi ya mililita 100 ya mvua jana ila, hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuelekea katika maeneo ya kaskazini na mashariki ya jimbo hilo hii leo.

Duru za pande hasimu nchini Kongo zimesema serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 wanajiandaa kwa mazungumzo ya ana kwa ana April 9.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.



Share