Australia ikoje kwa wahamiaji wenye ulemavu?

Patient using wheelchair moving in hospital courtyard

Migrants with disability are exposed to health screening processes that could impact their ability to stay in Australia. Source: iStockphoto / Vukasin Ljustina/Getty Images

Watetezi wa ulemavu na wataalam, wanasema unyanyapaa wa kitamaduni na sheria za uhamiaji, huwaacha wahamiaji wanao ishi na ulemavu wakiwa wame tengwa zaidi.


Unyanyapaa wa ndani na miiko ya kitamaduni, ni baadhi ya vizuizi vikubwa, kwa kuwasaidia watu wenye ulemavu ndani ya jumuiya zawa hamiaji.

“Hata kama walikuwa wanajua kuna misaada, [watu wenye ulemavu] kuna uwezekano hawata enda pata misaada hiyo kwa sababu, wanahisi wata jiaibisha,” Vanessa Papastavros, ni meneja wa mradi wakitaifa wa mradi wa ulemavu wa Speak My Language, ame eleza SBS Examines.

“Miongoni mwa walezi wa familia zenye watu ambao wana ulemavu, wangeweza mzuia pia mtu mwenye ulemavu kushiriki katika shughuli zaki jamii au uzoefu kama huo kwa sababu, walikuwa na woga wanaweza pata uzoefu wa unyanyapaa kutoka kwa wanachama wengine wa jumuiya.”
Mark Tonga, ni mhamiaji kutoka Fiji, amesema marafiki katika jumuiya yake, wali mchukulia tofauti baada yakupata jeraha la uti wa mgongo, ambalo lilimuacha na hali ya viungo vyote vya mwili kupooza, hali hiyo kwa kiingereza ina julikana kama tetraplegia.

“Watu huwa na wasiwasi wakati hawajui namna yaku chukulia hali hii,” alisema.

Ila amesema pia kuwa, jeraha lake silo linalo mzuia sana- bali ni ukosefu wa ufikiaji.
The world has a disability. We don’t have a disability.
“Panapo kuwa na jengo, na kuna watu ndani ya jengo hilo wanao hisi: ‘oh, watu wenye ulemavu hawawezi ingia hapa.’ Basi weka kifaa chaku saidia kuingia... na tuta ingia ndani!”

Kizuizi kingine kwa wahamiaji wenye ulemavu au hali sugu ya za afya ni, Mahitaji ya Afya ya Uhamiaji.

Hiki ni kipimo cha kiasi gani mahitaji ya matibabu ya mtu, yata gharimu jumuiya ya Australia.

Dkt Jan Gothard ni Wakala wa uhamiaji na mtetezi amesema, sharti hilo lina bagua.

“Inafanya mtu mwenye ulemavu ajihisi kuwa ametengwa,” alisema.

“Pia inatuma ujumbe kwa jumuiya kuwa watu wenye mazingira ya afya na ulemavu, ni mizigo kwa jumuiya.”

Makala haya ya SBS Examines yanatazama changamoto maalum, zinazo kabiliwa na wahamiaji wenye ulemavu nchini Australia.

Share