Key Points
- Voting is compulsory in Australia, but you have to be enrolled to vote.
- You must be an Australian citizen and at least 18 years of age to vote.
- You can enrol online or use a paper form.
- The AEC website offers information in language, and easy-read English guides.
hukusaidia katika maisha ndani ya nchi yako mpya Australia-
Uchaguzi wa shirikisho ni fursa ya kutoa maoni yako kwa kupiga kura, kuchagua serikali ya Australia.
Ni lazima kupiga kura nchini Australia, ila kuna baadhi ya mahitaji ambayo utahitaji timiza kwanza. Moja ya mahitaji haya ni kujisajili katika Tume ya Uchaguzi ya Australia (AEC).
Nastahiki kujisajili?
Hatakama kupiga kura ni lazima kwa wa Australia wengi, unastahili tazama ustahiki wako.
“Mtu yeyote ambaye ni raia wa Australia na ana miaka 18 au zaidi, anastahiki kujisajili na kupiga kura,” Evan Ekin-Smyth, msemaji wa AEC ametoa maelezo zaidi.
“Ila lazima usajiliwe kama unataka piga kura.”
Na stahili jisajili lini kupiga kura?
Wa Australia wapya wote hu hamasishwa kupiga kura wanapo kuwa raia ili, waweze toa maoni yao kwa siku za usoni za Australia.
Kawaida mwisho wa kujisajili ni wiki ya mwisho baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa. Kama umesajiliwa tayari, unawiki moja pia yaku toa taarifa zako mpya kama mabadiliko ya anwani au jina lako.
“Ila silazima usubiri tangazo la tarehe ya uchaguzi—unaweza fanya hivyo sasa hivi,” Bw Ekin-Smyth amesema.
Kwa kweli, silazima usubiri hadi ufikishe miaka 18 kujisajili, Kath Gleeson, Naibu Kamishna wa Uchaguzi katika AEC, amesema.
“Unaweza kuwa kwenye sajili ya uchaguzi kuanzia umri wa miaka 16, ili uwe tayari kupiga kura utakapo fikisha miaka 18.”

MELBOURNE, AUSTRALIA - MAY 18: A view from entrance of a polling station during general elections to elect its parliament and prime minister in Melbourne, Australia on May 18, 2019. Source: Anadolu / Recep Sakar/Anadolu Agency/Getty Images
Jinsi ya kujiandikisha
Unaweza jisajili kwa kutumia fomu rahisi mtandaoni. Unaweza jisajili hata kwa kutumia simu yako janja. Enda kwenye .
Ukipenda, au kama hauna intanet, fomu za karatasi zinaweza patikana katika ofisi yoyote ya AEC. Unaweza piga simu kwa namba hii 13 23 26 kupokea fomu hiyo kupitia posta.
Itabidi uthibitishe utambulisho wako, kwa hiyo weka utambulisho wako tayari. Hakuna haja yaku ambatanisha taarifa hiyo, ila itabidi uitaje.
Bi Gleeson amesema ushahidi wa utambulisho unaweza chuka umbo tofauti na, kuna taarifa nyingi katika lugha tofauti kwenye .
“Watu wengi hutumia leseni zao zaku endesha gari ila, unaweza tumia pia pasi au kadi yako ya Medicare,” amesema.

A ballot box is seen inside the voting centre at Collingwood in Melbourne, Saturday, October 14, 2023 Credit: CON CHRONIS/AAPIMAGE
Raia wapya watahitaji pia cheti chao cha uraia kujisajili.
Kama hauna aina yoyote ya utambulisho, au kama ume ipoteza, ni muhimu uiombe mapema sana. Mida ya kusubiri kwa kutolewa kwa vitambulisho, inaweza tofautiana kutoka mamlaka moja hadi nyingine na katika baadhi ya kesi inaweza chukua wiki nne.
Nastahili jisajili kwa kila uchaguzi?
Unapokuwa kwenye sajili ya kupiga kura, unaweza piga kura katika chaguzi yoyote ya shirikisho, jimbo au katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hii ndiyo sababu ni muhimu kuhakikisha taarifa zako ni sahihi.

Social media, connection and woman typing on a phone for communication, app and chat. Web, search and corporate employee reading a conversation on a mobile, networking and texting on a mobile app Credit: Delmaine Donson/Getty Images
Je niki hama ninako ishi itakuwaje?
Una wiki moja baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa, kuhakikisha kuwa taarifa yako ni sahihi.
“Tuta tuma vikumbusho tukipokea data inayo maanisha ume hama unako ishi, kwa mfano,” Bw Ekin-Smyth amesema.
“Ila ni muhimu unapo hama unako ishi, au unapo badili jina lako, unastahili sasisha maelezo yako.”
Kama hauna uhakika kama uko tayari katika sajili ya kupiga kura, enda kwa au piga simu kwa namba hii 13 23 26 kupata msaada.
Nani anaweza nisaidia kujisajili?
Tovuti ya AEC’s inajumuisha miongozo ya kustahiki na kujiandikisha, ambayo imetafsiriwa katika lugha yako. Wanatoa pia huduma ya ukalimani kwa simu pamoja na ‘miongozo rahisi yakusoma’ iliyo andikwa kwa kutumia Kiingereza rahisi pamoja na vielelezo.
Vituo vya Rasilimali za Wahamiaji na huduma za usaidizi za tamaduni nyingi, ziko hapo kusaidia wapiga kura wa mara ya kwanza na, ku kusaidia kufanya usajili.
Kila raia mpya wa Australia anastahili jiamini kujisajili, anapo stahiki kupiga kura. Kumbuka, kura yako ita hesabiwa bila kujali wewe ni nani.
Je itakuwaje kama sijisajili?
Kupiga kura ni lazima nchini Australia, na kufeli kupiga kura kunaweza sababisha upewe faini. Ila, kuweka kando hoja kuwa lazima upige kura, pia kumbuka kuwa utakosa fursa yakutoa maoni yako kama hau jisajili.
au tembelea ofisi ya AEC kujisajili kupiga kura katika uchaguzi wa shirikisho wa 2025.
Jiandikishe au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Explained kwa taarifa za ziada na maelezo muhimu kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una maswali yoyote au mawazo ya mada? tutumie barua pepe kwa [email protected]