Taarifa ya Habari 16 Mei 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Kiongozi wa Upinzani wa Shirikisho Sussan Ley, amesema kuungana tenana wanawake itakuwa kipaumbele chake kama kiongozi wa Upinzani wa shirikisho.


Matokeo mabaya ya upinzani katika uchaguzi wa shirikisho, yame zua shutma kuwa chama cha Liberal hakina mahusiano tena na Australia ya kisasa.

Kiongozi wa Victoria, Jacinta Allan, amesema bajeti ya jimbo hilo itakayo tolewa wiki ijayo, itajumuisha $152.3 milioni kuongeza kambi, michezo na mfuko wa ziara kwa wanafunzi wa shule za Victoria. Serikali ya Labor ya jimbo hilo imesema katikati ya shinikizo za gharama ya maisha, uwekezaji huo uta hakikisha kila mwanafunzi anaweza hudhuria kambi za shule, ziara nakushiriki katika michezo na wanafunzi wenza.

Naibu Rais wa zamani wa Kenya Rigathi Gachagua amezindua chama kipya cha DCP, akiahidi haki kwa wote na kushutumu mwelekeo wa chama tawala cha UDA ambacho alikuwa sehemu yake kabla ya kufarakana na Rais William Ruto. Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, ameanza ukurasa mpya wa kisiasa kwa kuzindua chama kipya kwa jina Democratic Citizen Party (DCP), akitaja kuwa ni jukwaa la kidemokrasia la kuwasikiliza Wakenya wote bila ubaguzi. Uzinduzi huo unakuja wakati Gachagua anazidi kujitenga na chama tawala cha UDA kilichomsaidia kuingia madarakani mwaka 2022.

Viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, wamelikosoa jeshi la polisi nchini humo kwa kile wanadai maofisa wake wanatumika vibaya kuminya upinzani baada ya kiongozi wake mwingine wa juu kukamatwa katika uwanja wa ndege. Usiku wa kumakia jana idara ya polisi ilimkamata naibu katibu mkuu wa chama hicho Amani Golugwa, katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam, kabla ya kuabiri ndege kuelekea Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa baraza la vyama vya siasa. Hata hivyo taarifa za kukamatwa kwake zilikuja kufahamika baadae kupitia kwa wasamaria wema waliomuona akikamatwa, ambapo baada ya shinikizo, polisi walitoa taarifa ya kukiri kumshikilia, wakidai wanataarifa fiche amekuwa akisafiri kinyume cha utaratibu.

Share