Gavana Mkuu amekabidhi Tume ya Uchaguzi ya Australia taarifa, inayo mpa Kamishna wa Uchaguzi amri ya kuandaa uchaguzi mkuu. Uchaguzi huo ulitangazwa Ijumaa iliyopita na bunge la 47 kuvunjwa ila, utoaji wa taarifa ni mwanzo rasmi wa uchaguzi. Hata kama taarifa hiyo imetolewa, haitachukuliwa kama imetolewa hadi saa kumi na mbili jioni ya leo.
Serikali ya Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo, inarejelea mashauriano ya kitaifa ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, yaliyoanza wiki moja iliyopita, na kususiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa wa upinzani.
Mchezaji gofu wa Australia Min Woo Lee, ameshinda kombe lake la kwanza la P-G-A, katika mechi ya wazi ya Houston,Texas.