Key Points
- The land is an inseparable part of First Nations peoples, forming their identity and sense of belonging.
- The connection stems from the stories that have been passed down through generations.
- One should only visit sacred sites with the knowledge of the site and its significance.
Wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait wame ishi Australia kwa angalau miaka elfu 60,000 waki kabiliana kwa mabadiliko ya mazingira.
Aunty Deidre Martin ni mwanamke kutoka ukoo wa Walbanga la taifa la Yuin. Ni kiongozi anaye heshimiwa pamoja nakuwa mlinzi wa ugunduzi waki Aboriginal anaye fanya kazi na Mbuga za taifa, pamoja na Huduma ya Wanyama katika nchi ya jimboni New South Wales.
Kwa Shangazi Deidre, ardhi si mali yaku milikiwa ila sehemu ambayo hawezi tengwa nayo, inayo hitaji heshimiwa nakulindwa.
We don’t and never will own the land. We have a role to protect the land. Our Country to land is what provides us with food, water, shelter, only to name a few.Aunty Deidre Martin
“Ardhi ni istilahi ila, inapita katika mishipa yetu yote. Ni pumzi yetu ya kwanza na itakuwa pumzi yetu ya mwisho,“ amesema.
Aunty Deidre Martin is an Aboriginal discovery ranger. Credit: Aunty Deidre Martin.
“Ninapo enda nyumbani kutoka Sydney, ninapo karibia kona ya Kiama huwa natazama pwani na hisia yakuwa sehemu huniteka na huwa nafikiria.... Niko nyumbani,” ali ongezea.
Desmond Campbell, ni mwanaume mwenye fahari kutoka ukoo wa Gurindji na Alawa-Ngalakan kutoka Wilaya ya Kaskazini, ame elezea hisia sawia na hizo anapo rejea katika ardhi yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa , ambayo kwa sasa iko Sydney, amesema huwa ana jawa hisia anapo fikiria kuhusu kuwa katika nchi yake.
“Hatakama haku kuwia hapo, nikama tulikuwa hapo jana. Ni sehemu tunayo fahamu nakuhisi salama. Unahisi nikama uko katika sehemu ambako unaweza jihisi huru kuwa kama mu Aboriginal,” Bw Campbell ame elezea.
Wakati muunganisho kwa nchi yake unaendelea kuwa imara licha ya umbali, Bw Campbell ame sisitiza umuhimu wakurejea mara kwa mara katika nchi yamababu zake, situ kwa kuendeleza utamaduni na lugha yake ila pia, kwa sababu ya muunganisho waki roho ambayo uhusiano huo hukuza.
“Huwa ina nijaza, huwa inajaza moyo wangu. Ina niruhusu kuweza kuishi katika sehemu kama Sydney na kufanya kazi katika shirika kama Welcome to County... Nahitaji hifadhi tamaduni na lugha yangu, pamoja nakuwa na uadilifu huo. Na naweza fanya hivyo tu kwa kwenda nyumbani mara kwa mara,”alisema.
CEO of Welcome to Country, Desmond Campbell. Credit: Desmond Campbell.
Hadithi kuhusu ardhi
Muunganisho huo unatoka katika hadithi zilizo elezwa katika vizazi, Bw Campbell ame elezea.
Ameongeza kuwa kutegemea na ardhi unako toka, hadithi, mioyo na miunganisho inatofautiana.
“Upande wangu wa Gurindji, ambao ni upande wa babangu, niwa nchi ya jangwa. Wanyama wanatofautiana, misimu ni tofauti kwa hiyo hadithi zina tofautiana pia [kwa upande wa mamangu].”
Bw Campbell amesema hadithi hizi zilichanganywa na ujuzi pamoja na mafunzo kuhusu ardhi, kama sehemu na mahali na chaku winda na madhara yakucheza na moto katika msimu usio sahihi.
Bradley Hardy ni mwanaume kutoka ukoo wa Ngemba, Ualarai, Kooma na Kamilaroi yeye pia ni mlinzi wa kisasa wa ambazo ziko katika mto Barwon.
Ame elezea mto huo kama "damu yake na utambulisho".
Bw Hardy anaendelea kusema hadithi na historia za ardhi yake, akifanya kazi kama mtu anaye toa mwongozo wa ndani katika makumbusho ya .
Amesema, lazima aendelee kuhakikisha hadithi hizo zina endelea kuwa hai kwa kuzichangia katika kizazi kijacho.
“Daima ziara hai ni husu, ila inahusu kuwa enzi wazee wangu, kuchangia na vijana pamoja naku andaa mitandao kwa vijana waendelee kuchangia historia yetu na dunia, na ni wajibu wetu kufanya hivyo,” Bw Hardy ame elezea.
Bradley Hardy and Brewarrina Aboriginal Fishing Traps. Credit: Bradley Hardy.
Kuelewa sehemu takatifu
Mitego ya samaki yaki Aboriginal katika Brewarrina ni miongoni mwa miundo kongwe ya ujenzi duniani. Imeundwa kwa mawe ambaye yame wekwa kimkakati katika miundo ya U na C, si tu kuongoza naku nasa samaki ila pia, kuruhusu baadhi ya samaki kupita nakuendeleza mzunguko wazo wa maisha, Bw Hardy ame elezea.
Hapo ndipo kabila nyingi zili jumuikia pia.
It’s a sacred site, we’ve got to try and protect it. It’s mainly for our people. Our main duty is to not only tell people about them and keep it evolving amongst our young people, but for the world [to know] these are special places.Bradley Hardy
Shangazi Deidre ame elezea pia umuhimu wakujua sehemu takatifu na umuhimu wazo kabla yaku zitembelea.
“Ni maeneo yenye ujuzi ambayo hauwezi tembelea hadi, upate ujuzi, kwa mfano maeneo ya wanaume na wanawake,” ame elezea.
Silhouette image of First Nation Australian aboriginal people, father and son, going to hunt seafood in Cape York, Queensland, Australia. Credit: Rafael Ben-Ari/Getty Images Credit: Rafael Ben-Ari/Getty Images
Shangazi Deidre amesema ni wajibu wake kuelimisha jumuiya kuhusu maeneo haya takatifu, na kwa kweli huwa ana furahia kuchangia ujuzi wake na wageni.
Kuingia kwa undani zaidi katika katika ardhi ya watu wa mataifa ya kwanza nakuelewa umuhimu wayo kunaweza onesha utajiri wa ujuzi. Hata hivyo, ni muhimu kuelekea katika maeneo takatifu yakiasili kwa heshima na kuomba mwongozo kutoka jumuiya za wenyeji au baraza za ardhi.
“Iwe ni mitego ya samaki au historia zingine katika sehemu tofauti, tunataka watu waende na wapate ukweli wa historia yetu. Tunawataka watu waje na wajifunze kuhusu hivi vitu ila pia wawe makini na waheshimu mambo yetu pia,” Bw Hardy ame ongezea.