Bajeti ya shirikisho inapo jiri chini ya wiki nane kabla ya uchaguzi mkuu, serikali ya shirikisho imejipata katika nafasi ngumu, ikijaribu kusawazisha vipaumbele vyake, na kudhibiti ujumbe.
Bajeti kwanza kabisa zina husu serikali kuwa ambia watu jinsi wata tumia hela zao za ushuru.
Na kuna taarifa nyingi zaku pigia hali hiyo debe kuelekea kutangazwa kwa bajeti, serikali ikiwa haina haya kuwa eleza wa Australia kuhusu ahadi kubwa za matumizi, inapokuja kwa Medicare, Miundombinu, Makaazi miongoni mwa vitu vingine, wanapo jiandaa kuelekea katika vituo vyakupiga kura.