Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw Matt Gitau alifunguka kuhusu baadhi ya changamoto yeye na wanajumuiya wake wame kuwa waki kabili.
Bw Matt, alifunguka pia kuhusu nia yaku andaa hafla yakuwaleta wanajumuiya pamoja kujadili maswala ya afya ya akili kupitia hafla yakutembea naku kimbia kwa takriban kilomita 7.
Hafla hiyo itafanyika katika viwanja vya Sydney Olympic Park, Jumamosi 15 Machi 2025 kuanzia saa sita mchana kwa masaa ya Mashariki Australia.
Kwa maelezo zaidi kuhusu tukio hili na kama ungependa kuwasiliana na Bw Matt na wakenya wenza, unaweza wapata katika mtandoa wakijamii wa Instagram uki andika: Kenyacommunity_nsw