Kunyanyaswa kwa wa Islamu ni aina ya ubaguzi wa rangi unao lenga Uislamu au Uislamu unao tambulika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sajili ya Chuki dhidi yawa Islamu nchini Australia Dkt Nora Amath amesema ripoti za matukio ya Kunyanyaswa kwa wa Islamu, zime ongezeka kwa zaidi ya asilimia 1300 tangu Oktoba 7 mwaka jana.
Ila amesema pia kuwa matukio mengi huwa haya ripotiwi.
“Kwa bahati mbaya kuna baadhi yawa Islamu wanao amini kuwa, hii ni sehemu yakuwa Muislamu hapa- kuvumilia na kukabiliana na chuki."
Dkt Amath amesema pia kuwa Kunyanyaswa kwa wa Islamu, kwa masikitiko kumekuwa sehemu ya maisha ya kila siku yawa Islamu wengi nchini Australia- haswa wanawake ambao ni takriban asilimia 80 yawa athirika.
"Kila mwanamke Muislamu ambaye nime ongea naye, na hiyo ni asilimia 100, amepata tukio na, hata hivyo hawaja iripoti," ali eleza SBS Examines.
Dkt Amath amewahimiza watazamaji, waathiriwa na wanao waunga mkono waripoti tukio lolote la Unyanyasaji wa waislamu kwa sajili hiyo.
"Tunataka ujue kuwa ni haki yako kuripoti, haustahili ishi na swala hili na haufai kubali hali hii nchini Australia."
Makala haya ya SBS Examines yanachunguza uzoefu wa Kunyanyaswa kwa wa Islamu nchini Australia.